.
7th February, 2019
Kamati ya bunge la taifa inayohusika na masuala ya kilimo imemwagiza waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri na mwenzake wa fedha Henry Rotich kufika mbele ya kamati hiyo siku ya jumatatu ili kueleza sababu za kuwepo uhaba mkubwa wa mbolea ya bei nafuu kwa wakulima. Kamati hiyoimesema uhaba wa mbolea wakati taifa linapojiandaa kwa msimu wa upanzi wa mahindi huenda ukasababisha ukosefu mkubwa wa chakula. wabunge hao wametoa mwito kwa baraza la mawaziri kufanya kikao cha dharura ili kuzuia nchi kutumbukia kwenye janga la njaa