BONGO LA BIASHARA: Lilian Kanini afanya biashara ya kuuza nguo za wanawake wanene

KTN News Jan 29,2019


View More on KTN Leo

Ni mtaalamu wa huduma za ndege na uhusiano mwema. Baada ya kuwa katika ulingo huu kwa miaka 9, Lilian Kanini alisukumwa na wanawakewanene aliowaona ndegeni na mijini ulimwenguni alikozuru wakiteseka kupata nguoza kuwatosha. Mbali na hao alimshuhudia mamake vilevile akipata tabu iyohiyo kwa sababu ya ukubwa wake. Hili lilimfanya aache ajira yakekatika kampuni ya ndege ya Qatar aanze kuuza nguo.