Ripoti ya upasuaji wa mwili wa Kenneth Abom imewasilishwa kwa familia yake

KTN News Jan 22,2019


View More on KTN Leo

Hatimaye ripoti ya upasuaji wa mwili wa Kenneth Abom mwanafunzi wa chuo kikuu cha Strathmore imewasilishwa kwa familia yake. Uchuguzi huo sasa unaonyesha kuwa abom alifariki kutokana na majeraha kadha wa kadha kwenye kichwa chake, kifuani na sehemu nyinginezo.familia ya marehemu inazidi kushikilia kuwa kifo cha kijana wao kina uhusiano wa karibu na kushambuliwa kwake na msanii wa kufokafoka henry ohanga maarufu kama octopizzo. Wakati huo huo viongozi wa vyuo vikuu wameongoza maandamano jijini nairobi hii leo kuishinikiza serikali kutoa majibu kwa mauaji kadha wa kadha miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.