Sarakasi Kajiado Kusini baada ya mama kujaribu bila mafanikio kumuoza bintiye mwenye Miaka 12

KTN News Jan 18,2019


View More on Leo Mashinani

Palitokea sarakasi huko kajiado kusini baada ya mama mmoja kujaribu bila mafanikio kumuoza binti wao mwenye umri wa miaka kumi na miwili. Maafisa wa usalama walimuokoa msichana huyo wa darasa la nne katika kijiji cha Eselenkei,ambaye  anadaiwa alipangiwa kuolewa na moran mmoja kwa jina Lemunja.  Leah Kalenyi ambaye ni mamake msichana huyo pamoja na moran huyo walikamatwa na kushtakiwa katika mahakama ya Loitoktok mbele ya hakimu Mathias Okuche