Wanawake wafaulu katika kilimo kaunti ya Wajir | Mwako mpya Wajir

KTN News Dec 17,2018


View More on KTN Leo

kaunti ya Wajir, sawa na lilivyo eneo zima la Kaskazini Mashariki, ni eneo kame lisilo na uwezo wa kilimo cha mazao shambani. Kiangazi, njaa na ukosefu wa mvua ni baadhi ya mambo ambayo hutumiwa kuelezea hali ya wajir. Lakini wapo wanawake ambao kupitia ubunifu na mikakati mahsusi, wamefaulu katika kilimo na kuzalisha lishe mbadala kupitia kilimo cha kisasa kwenye mahema maalum almaarufu green house, na sasa wanafurahia pato nono litokanalo na juhudi zao.