17th December, 2018
Mahakama ya Eldama Ravine kaunti ya Baringo imempa mwalimu wa michezo ambaye alishtakiwa kwa kosa la kujaribu kumuua mwalimu mkuu wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Toniok kifungo cha miaka arobaini gerezani. Hii ni baada ya mahakama kumpata na hatia. Katika uamuzi wake Hakimu Mkuu wa mahakama ya Eldama Ravine Judiscaster Nthuku amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ulikuwa wa kutosha na ulidhihirisha jinsi Andrew Omdondi alivyotekeleza uovu huo. Inadaiwa mnamo Oktoba kumi mwaka 2017, katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Toniok, Omondi akiwa amejihami kwa nyundo alijaribu kumuua mwali mkuu Sally Nabori kwa kumgonga kichwani.