12th December, 2018
Mnamo Oktober 1964, serikali ya rais Mzee Jomo Kenyatta tayari ilikuwa na changamoto za kiusalama kutokana na wapiganaji waliotajwa kuwa mashifta kaskazini mashariki mwa kenya. Wapiganaji hao walitaka kujiondoa kutoka kwa ramani ya Kenya. vita vya shifta vilivyoanza mwaka wa 1963 zilihitaji maaskari zaidi, na ikabidi rais Kenyatta kuamuru kuajiriwa kwa makurutu wa jeshi watakaopambana na changamoto hiyo ya usalama kaskazini mwa Kenya. Clisantus aaron ojode, ni mojawapo wa ma askari waliochukuliwa mwezi wa Oktoba 1964, kusaidia taifa changa la Kenya kupamabana na utovu wa usalama.