Unajisi Hospitalini: Mwanamke anajisiwa na mlinzi hospitalini baada ya kujifungua

KTN News Dec 05,2018


View More on KTN Leo

Mlinzi mmoja katika Hospitali ya Rufaa ya Marsabit ametiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kumnajisi mama mmoja aliyejifungua kwenye hospitali hiyo. Jamaa huyo aliyefahamika kwa jina Guyo Bukicha alikamatwa na maafisa wa kitengo cha ujasusi siku tatu zilizopita baada ya kudaiwa kutenda unyama huo kwenye wodi ambamo mama huyo alikuwa amejifungua mtoto ambaye umiri wake wa kuzaliwa ulikuwa haujatimia. Uongozi wa hospitali hiyo umelaumiwa kwa kitendo hicho.