Gavana Sonko akemea Ubomoaji Woodely; asema ni haramu

KTN News Dec 05,2018


View More on KTN Leo

Wafanyabiashara katika eneo la Woodley kwenye barabara ya Ngong wamejipata kwenye njia panda baada ya genge la vijana kuamkia ubomozi wa vibanda vyao pasi na ilani yoyote. Japokuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko amelaani ubomozi huo alioutaja kuwa haramu wafanyabiashara hao wangali na maswali tele baada ya vijana hao hao kuweka uwa wa mabati chini ya usimamizi wa maafisa wa usalama.