.
28th November, 2018
Wanachama wa Bunge la Taifa kwa pamoja wameafikiana kuzuia juhudi zozote za Idara ya Upelelezi wa Jinai au Tume ya Kupambana na Ufisadi nchini kuwachunguza wabunge waliopokea hongo ili kutupilia mbali ripoti ya uchunguzi wa sukari ya magendo nchini. Katika njama ya kusafisha na kutakasa heshima ya bunge, wanachama hao walifanyia marekebisho ripoti ya kamati ya mamlaka ya Bunge la Taifa iliyoongozwa na spika Justin Muturi.