.
12th November, 2018
Takriban watu 2000 wametiwa nguvuni kwenye msako ambao umefanyika hii leo katika harakati za kuleta nidhamu katika sekta ya uchukuzi nchini. Waziri wa usalama daktari Fred Matiangi, amesema serikali haitalegeza kamba katika kuhakikisha sheria na kanuni za barabarani zinazingatiwa na kuheshimiwa. Ameonya kuwa vyama vya ushirika ambavyo vimekataa kutoa huduma kwa wasafiri huenda vikapoteza leseni zao. Isitoshe amesema hawataruhusu vitisho kutoka kwa yeyote. Wakati uo huo, inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinnet amesema polisi hawatasaza yeyote atakayekiuka sheria.