Masilahi ya walemavu: Denitta Ghati atoa wito kwa Rais, ataka bodi iundwe katika National council

KTN News Nov 08,2018


View More on KTN Leo

 

Mbunge wa kuteuliwa anayeshughulikia Masuala ya Walemavu, Dennitah Ghati, ametoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kuteua haraka iwezekanavyo wanachama wa bodi Inayoshughulikia masuala ya walemavu.  Mbunge huyo pia Ametaka masuala ya walemavu kupewa kipaumbele katika Serikali za kaunti ili wajumuishwe na wakenya wengine. Idadi ya walemavu nchini Kenya inakisiwa kuwa watu milioni 6.5.