Wanafanyi kazi wa Commitee to Protect Journalists(CPJ) waachiliwa huru nchini Tanzania

KTN News Nov 08,2018


View More on KTN Leo

 

Serikali ya Tanzania kupitia Idara ya Uhamiaji ya nchi hiyo imethibitisha kuwaachia huru wafanyakazi wawili wa kamati maalumu ya Kutetea Wanahabari Duniani (cpj) waliokamatwa na idara hiyo hapo jana jijini Dar Es Salaam. Wafanyakazi hao Angela Quintal na Muthoki Mumo wanatuhumiwa kwa kukiuka masharti ya viza yao ambayo ni ya matembezi na badala yake wamekuwa wakifanya mikutanao na wanahabari wa nchi hiyo.