.
31st October, 2018
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto, wamewataka watahiniwa wa mtihani wa KCPE kuonesha ukakamavu wanapoukabili mtihani wao wa taifa.
Wakiongea katika shule tofauti walipongooza shughuli ya kufungua kontena za mitihani kwa siku ya pili ya mtihani huo, viongozi hao waliahidi kwamba kila mtahiniwa anayeshiriki mtihani huo atapata nafasi ya kujiunga na shule ya upili.