.
30th October, 2018
Katibu mkuu wa chama cha wauguzi nchini Seth Panyako leo hii alifikishwa mahakamani na kushtakiwa na kosa la kuchochea mgomo katika hospitali ya Kenyatta. Panyako alishtakiwa pamoja na wanachama Joseph Wanyoike na Evans Mwendwa. Watatu hao waliyakanusha mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya shillingi elfu hamsini.