Makala maalum: Rais mstaafu Daniel Moi aliongoza taifa hili kwa miaka 24

KTN News Oct 10,2018


View More on KTN Leo

Rais mstaafu Daniel Moi aliongoza taifa hili kwa miaka 24. Wakati wa uongozi wake, Moi alitambulika kama kiongozi mchapa kazi na siku haingalipita bila wananchi kufahamishwa pilka pilka za rais.

 Licha ya hayo, je wajua mwanzo wa mwaka 1995 taifa lilikumbwa na kiwewe pale Moi alikosa kuonekana hadharani kwa wiki moja pasi na habari kuhusu alikokuwa kiongozi wa taifa?  

Naam, hiyo ilikuwa mojawapo ya mbinu za kisiasa za Moi kukabiliana na joto la siasa za upinzani wakatihuo.  Wakenya wanapoadhimisha sikukuu ya Moi, mwanahabari wetu wa masuala ya kisiasa, Patrick Amimo, alikita hema kwenye maktaba na kutuandalia taarifa ya kumbukumbu kadha za Moi.