9th October, 2018
Wakaazi wa eneo la maparsha kaunti ya kajiado wamelipa shirika la wanyama pori kws makataa ya siku 7 kuwaondoa ndovu ambao wamekuwa wakiwahangaisha au la wachukue hatua ya kuwaangamiza. Wakazi hao wenye ghadhabu wamelalamikia kuwa ndovu hao wamekuwa wakiwashambulia na kuharibu mimea yao huku shirika hilo likionekana kupuuza malalamishi yao. haya yanajiri siku 2 tu baada ya simba
kudaiwa kuwashambulia na kuwaua zaidi ya ngombe 10 eneo hilo. Vile vile inadaiwa baadhi ya wanafunzi wameshindwa kwenda shuleni kwa masomo yao kwa kuhofia kushambuliwa na wanyama hao hatari. wakazi hao walitembea mwendo wa zaidi ya kilomita 40 hadi mjini ilbisil ili kuwasilisha malalamishi yao.