Mauaji ya mwanamke katika eneo la Kilimani-Nairobi yachunguzwa

KTN News Sep 21,2018


View More on Dira ya Wiki

Maafisa wa usalama wameanzisha uchunguzi kufuatia mauaji ya mwanamke mmoja eneo la Kilimani hapa jijini Nairobi. 

Mwili wa mwanamke huyo anayetambulika kama Monika Kimani ulipatikana na nduguye alhamisi nyumbani kwa mwenda zake.

Nduguye marehemu amesema kuwa alikwenda kumjulia hali Monika na akaupata mwili wake kwenye bafu ukiwa na majeraha ya kisu shingoni. 

OCPD wa Kilimani Michael Mushiri amesema kuwa marehemu aliuwawa kwa njia ya kutatanisha na polisi wameanzisha uchunguzi. 

Mwili wa mwenda zake ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Chiromo.