Mbunge wa zamani wa eneo la Nyatike azungumzia mzozo wa Migingo

KTN News Sep 14,2018


View More on KTN Mbiu

Mbunge wa zamani wa eneo la Nyatike Edick Omondi Anyanga ametoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta kufanya mazungumzo na rais Yoweri Museveni wa Uganda kuhusiana na mzozo wa kisiwa cha Migingo. 

Akizungumza akatika eneo la Wath Ong'er katika kaunti ya Migori, Anyanga amesema kwamba inakera kuona askari wa Uganda wakichukua usukani katika ardhi ya Kenya, huku Kenya inajivunia kuwa taifa huru.