Rais Uhuru Kenyatta apendekeza bunge kupunguza ushuru kwa bidhaa za mafuta

KTN News Sep 14,2018


View More on KTN Mbiu

Rais Uhuru Kenyatta amehutubia taifa alasiri hii na kusema kwamba amependekezea bunge kupunguza ushuru wa thamani ya ziada kwa bidhaa za mafuta kutoka asilimia kumi na sita hadi asilimia nane. 

Rais amesema kwamba anaelewa mzigo wa gharama ya maisha ambayo Wakenya wanapambana nayo lakini akasisitiza kwamba ushuru huo unatokana na mswada uliopitishwa na bunge mwaka wa 2013. 

Aidha rais amesema kwamba kutokana na katiba mpya, nyadhifa kadhaa za uwakilishi zilibuniwa, na ndiposa gharama ya matumizi ya fedha imeongezeka.