Mwanamke mmoja wa miaka 35 ajaribu kuumza mtotoye kwa Kshs.1,200

KTN News Sep 11,2018


View More on KTN Leo

Mwanamke mmoja wa miaka 35 amekamatwa katika Hospitali ya Level 5 mjini Nakuru, baada ya kujaribu kuumza mtoto wake wa wiki tatu, mda mchache baada ya kupewa ruhusa kwenda nyumbani. Ann Wangui mkaazi wa njoro, alijaribu kumuuzia mtoto huyo dorcas nanjala kwa shilingi 1200/. Inasemekana mtoto wa dorcas alifariki wakiwa hospitalini humo mda mchache baada ya kujifungua. Wangui  alimuuzia  nanjala  malaika huyo, akidai kuwa ada hio ni ya kumuangalia mtoto huyo akiwa hospitalini kwa kipindi cha wiki tatu, baada ya kuzaliwa. Wangui anazuiliwa na maafisa wa polisi huku uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukiendelezwa.