Aliyekuwa Mwakilishi wa Wadi Lawrence Mula alifikishwa mahakama kufuatia kifo cha Sharon

KTN News Sep 10,2018


View More on KTN Leo

Huku hayo yakijiri, aliyekuwa Mwakilishi wa Wadi ya Kanyadoto Lawrence Mula alifikishwa mahakama ya Kisii kuhusiana na kesi ya mauaji ya Sharon Otieno. Upande wa uongozi wa mashtaka walisema kwamba  mshukiwa ni mojawapo wa washukiwa wakuu ambao watasaidia kukwamua muuaji wa marehemu. Pia wamesema kwamba kundi la wachunguzi kutoka nairobi watahitaji mda zaidi kumhoji mshukiwa huyo wa nne, hakimu mkuu wa mahakama ya kisii aliitika wito wa upande wa mashtaka wa mda zaidi kukusanya ushahidi wao. Mula alishikwa na polisi hapo jana, na atasalia katika rumande ya kituo cha polisi cha kisii hadi tarehe 24 septemba ili polisi waweze kufanya uchunguzi.