Ababu asema eneo la Budalangi halitafutwa

KTN News Sep 09,2018


View More on KTN Mbiu

Katibu wa maswala ya usimamizi katika wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ababu namwamba amewataka wakaazi wa eneo la budalangi kuondoa shaka kwamba eneo bunge lao huenda likafutwa katika tathmini ijayo ya mipaka ya maeneo bunge na tume ya uchaguzi nchini iebc. namwamba ambaye aliwahi kuwa mbunge wa eneo hilo amesema ameiandikia barua iebc kuikumbusha kuhusu kifungu cha 89 cha katiba kinachotoa mwelekeo  kuhusu kubuniwa au kuvunjwa kwa maeneo bunge kwa kuzingatia utamaduni, kabila na historia ya maeneo.