Mali ya kampuni ya Sukari ya mumias imeanza kupigwa mnada

KTN News Sep 05,2018


View More on Leo Mashinani

Mali ya kampuni ya Sukari ya mumias imeanza kupigwa mnada baada ya kampuni hiyo  kushindwa kulipa malimbikizi ya mishahara na madeni ya wafanyikazi wake.  Wakulima wa kiwanda  hicho wameapa kuzuia mali ya kampuni hiyo kupigwa mnada ikiwemo magari ambayo tayari yameorodheshwa. Kuanzia juzi wakulima wamekuwa wakiwazuia mawakala hao kuingia kiwandani humo kwa madai kuwa wamekiuka makubaliano ya kusubiri malipo hadi kiwanda hicho kipate muthamini.