Mahakama kuu imekataa kusimamisha matumizi ya ushuru wa asilimia 16

KTN News Sep 04,2018


View More on KTN Leo

Kutoka mahakamani ni kwamba kuwa mahakama kuu imekataa kusimamisha matumizi ya ushuru wa asilimia 16 kwa bidhaa za petroli. Mahakama hio imetoa uamuzi alasiri hii, na kusema kwamba shughuli ya bunge haijakamilika hadi rais kenyatta atie sahihi au kukataa kuitia saini mswada huo.  Kutumika kwa ushuru huo kumepingwa vikali na wakenya mbalimbali,haswa kwa kuwa inapandisha gharama ya maisha, kando na kumlimbikizia mkenya wa kawaida ushuru huo.