Wakaazi wa Thika wamepata mradi wa unyunyiziaji maji mashamba

KTN News Sep 03,2018


View More on KTN Leo

Wakaazi wa Ngoliba na Maguguni katika mji wa Thika Kaunti ya Kiambu wana kila sababu ya kufurahia baada ya kufufuliwa kwa mradi wa unyunyiziaji maji mashamba ambao unatarajiwa kuyabadilisha maisha yao pakubwa. Mradi huo ulikuwa umeanzishwa miaka 5 iliyopita lakini ukazagaa baada ya fedha zipatazo shilingi milioni 400 kufujwa na waliokuwa wakiusimamia.