Richard Lesiyampe amekamatwa katika operesheni ya kupambana na ufisadi

KTN News Aug 30,2018


View More on Leo Mashinani

Katibu wa kudumu katika wizara ya kiliomo richard lesiyampe amekamatwa katika operesheni inayoendelea ya kupambana na ufisadi katika idara mbali mbali serikalini. Lesiyampe alikamatwa leo asubuhi kuhusiana na madai ya kuidhinisha halmashauri ya mazao na nafaka NCPB kununua mahindi kwa matumizi ya mgao wa fedha ambazo hazikupaswa kufanya shughuli hiyo. Kadhalika meneja wa maswala ya fedha katika halmashauri hiyo Cornel Kiprotich amekamatwa na wote wanatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama ya kupambana na ufisadi baadaye.