Maabara ya LANCET imeruhusiwa kufanya vipimo vya damu

KTN News Aug 27,2018


View More on Sports

Maabara ya LANCET mjini Nairobi imeruhusiwa na shirika linalopiga vita utumizi wa dawa zilizoharamishwa duniani wada kufanya vipimo vya damu kwa uchunguzi. Maabara hiyo ambayo imekuwa ikifanyiwa majaribio kwa muda wa miezi tisa kwa ushirikiano wa tume ya maadili ya wanariadha aiu na wakfu wa wanariadha wa kimataifa iaf itakuwa ya kwanza katika kanda ya afrika mashariki kupewa kibali hicho. Shughuli yenyewe itang'oa nanga mwezi ujao huku ikitarajiwa kufanya vipimo kati ya 800 na 1000 kila mwaka.