Mbunge James Gakuya aachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni tano

KTN News Aug 23,2018


View More on KTN Leo

Mbunge wa Embakasi kaskazini James Gakuya aliyekamatwa Jumatano kuhusiana na matumizi ya takriban shilingi milioni 40 za CDF ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni tano au pesa taslimu shilingi milioni mbili. 

Gakuya na wengine 12 wanatuhumiwa na tume ya kupambana na ufisadi eacc kwa mashtaka 27 yanayohusiana na matumizi mabaya ya afisi na fedha za umma yakihusiana na zabuni za ujenzi wa barabara eneo bunge lake. 

Hakimu Felix Kombo wa mahakama ya Milimani alimwagiza Gakuya na washtakiwa wenza pia kuweka paspoti zao mahakamani kufikia Jumatatu Agosti 28.