'Wacheni kuzungumzia yaliyopita' Murkomen awaambia viongozi wa NASA

KTN News Aug 19,2018


View More on KTN Leo

Kiongozi wa wengi katika bunge la Senate Kipchumba Murkomen sasa amewashutumu viongozi wa upinzani kwa kujaribu kuhujumu  ushirikiano  uliopo baina ya rais Uhuru Kenyatta na kinara wao Raila Odinga.

Murkomen amesema kuwa ni jambo la kushangaza kwamba licha ya rais Uhuru Kenyatta kujiepusha na mjadala kuhusu yaliyopita viongozi hao wameendelea kumkosoa jambo ambalo amesema linaenda kinyume na maafikiano ya kuleta maridhiano nchini