Wakazi wa Isiolo walalamikia muda mrefu wa kujenga barabara

KTN News Aug 14,2018


View More on Leo Mashinani

Wakaazi wa eneo la kinna Kaunti ya Isiolo wanalalamikia muda mrefu unaotumiwa kujenga barabara ya gabartula?kinna?mulika, kutoajiriwa kwa vijana katika shughuli nzima ya ujenzi huo pamoja na kunyanyaswa kwa jamii hiyo na maafisa wakuu wa kampuni iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa barabara hiyo. 

Kulingana na wakazi hao, ni umbali wa kilomita sabini za barabara hiyoambazo zinafaa kujengwa, lakini ni umbali wa kilomita saba tu ambao umekamilikakwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja. Sasa wanahofia huenda shughuli hiyo ya ujenzi isikamilika katika muda uliokuwa unafaa wa miaka mitatu.