Evans Kidero afikishwa mahakamani ili kuyajibu mashtaka matatu ya ufisadi dhidi yake

KTN News Aug 09,2018


View More on KTN Leo

Aliyekuwa gavana wa Nairobi, Dr. Evans Kidero, amefikishwa mahakamani ili kuyajibu mashtaka matatu ya ufisadi dhidi yake. Kidero aliyekuwa pamoja na mtuhumiwa mwenza, Maurice Ochieng Kere, walifikishwa mbele ya hakimu Douglas Ogoti, na kuyakana mashtaka yote dhidi yao. Hata hivyo kidero aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni mbili pesa taslimu.