×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Polisi huko Donholm apatikana kajinyonga katika hali tatanishi

19th June, 2018

Polisi huko Donholm wanachunguza kifo cha mmoja wao aliyepatikan nyumbani kwake akiwa amejinyonga Koblo Patrick Macharia kutoka kituo cha polisi cha Soweto alistahili kurejea kazini mnamo jumanne asubuhi baada ya mapumziko. Hata hivyo saa za kuwasili kazini zilipofika wenzake wakakosa kumwona, walikata kauli ya kumpigia simu ili wafahamu hali yake. Lakini baada ya simu zao kukosa kupokelewa, waliamua kwenda nyumbani kwake. Hata hivyo iliwabidi wamsubiri bintiye aje aufungue mlango kwani ulikuwa umefungwa kwa ndani. Baadaye walipigwa na butwaa walipoupata mwili wa mwendazake ukining’inia katika chumba chake cha kulala.  Majirani wamemtaja kuwa mtu mpole na mpenda amani. Alikuwa akiishi katika nyumba za polisi za Donholm

.
RELATED VIDEOS