Mzozo watokota kiwanda cha maziwa Bungoma kufuatia kashfa ya Sh60M

KTN Leo | Tuesday 12 Jun 2018 8:50 pm

Mzozo unatokota katika kiwanda cha maziwa kaunti ya Bungoma kuhusu sakata ya ufisadi ya shilingi milioni 60 huku wakulima wa maziwa wakiapa kuendelea kupiga kambi katika afisi ya waziri wa kilimo kaunti hiyo wakimtaka kuingilia kati na kuhakikisha kuwa wanapata malipo ya maziwa yao wanayodai.