Mwanamke Laikipia atengeneza mapambo kutokana na taka za plastiki

KTN Leo | Tuesday 12 Jun 2018 7:41 pm

Uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki sio jambo geni nchini. Licha ya serikali kupiga marufuku mifuko ya plastiki, bado uchafuzi huo unashuuhdiwa. Lakini wafahamu kuwa taka hizo za plastiki na pia za khaki zaweza kutumika kutengeza mapambo kama vile ushanga na vipuli. Raquel Muigai alipata kukutana na mwanamke mmoja katika kaunti ya Laikipia anayefanya hivi na kutupambia makala ya Bongo la Biashara.