Jaji mkuu Maraga awahakikishia wanahabari uhuru wao

KTN Leo | Tuesday 12 Jun 2018 7:35 pm

Jaji mkuu David Maraga ameihakikishia jamii ya wanahabari nchini kuwa idara ya mahakama italinda uhuru wa wanahabari mradi tu wazingatie kanuni zilizowekwa wanapotekeleza majukumu yao. Maraga alisema hayo katika kikao  cha jukwaa la wahariri nchini kilichokuwa kikitathimini mahusiano uanahabari, demokrasia na  uhuru wa kujieleza miongoni mwa mambo mengine.