26th May, 2018
Kiongozi wa NASA Raila Odinga amesema serikali inatakiwa kukabiliana na ufisadi kwa dhati. Raila ambaye alikuwa Magharibi mwa Kenya ameshikilia kuwa mapatano kati yake na Rais Uhuru Kenyatta yanastahili kutimiza dhamira ya kumaliza ufisadi nchini. Hayo yanajiri huku viongozi wakiwataka rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kuwajibika kuhusu sakata za NYS na NCPB.