5th April, 2018
Serikali ya kaunti ya Migori imeanza mpango wa kupanda miti katika shule za msingi kama njia ya kuimarisha mazingira. Akizungumza katika uzinduzi huo mwenyekiti wa Migori rottary club Ojwando bobo amesema kuna mpango huo wa kupanda miti miche milioni moja katika shule 800 za msingi katika muda wa mwaka mmoja. Siku ya jana wanafunzi wa shule ya msingi ya relief academy walipanda miche 400 katika mpango huo kwa jina green Migori.