Chama cha wanahabari wa michezo kimepigwa jeki baada ya LG kutoa wa shillingi milioni sita

Sports | Tuesday 13 Feb 2018 7:41 pm

Chama cha wanahabari wa michezo kimepigwa jeki baada ya kampuni ya LG kutoa  ufadhili wa shillingi milioni sita ambazo zitawezesha chama hicho kutuza wachezaji bora kila mwezi katika ligi kuu ya kandanda nchini. Chama hicho kitamtuza mchezaji bora kila mwezi na mchezaji huyo atapokea televisheni. Kampuni hiyo ya LG pia itasaidia chama hicho kuandaa tuzo za mchezaji bora mwishoni mwa msimu.