UNESCO kwa ushirikiano na Microsoft Africa iliandaa warsha ya siku ya kimataifa ya wanawake

KTN Leo | Tuesday 13 Feb 2018 7:37 pm

Kitengo cha elimu, sayansi na tamaduni katika umoja wa mataifa, UNESCO kwa ushirikiano na Microsoft Africa iliandaa warsha ya siku ya kimataifa ya wanawake wanaokumbatia taaluma ya sayansi.  Warsha hiyo inanuia kuwaleta wanawake katika taaluma ya sayansi pamoja na kuwapa changamoto watoto wa kike katika shule za sekondari kukumbatia sayansi kama taaluma.  Kwa miaka mingi masomo ya sayansi yameonekana kama ya kiume lakini warsha ya jana inalenga kufutilia mbali kasumba hiyo.