Chama cha ANC nchini Afrika Kusini kimemtaka rais Jacob Zuma kujiuzulu mara moja

KTN Leo | Tuesday 13 Feb 2018 7:21 pm

Chama cha ANC nchini Afrika Kusini kimemtaka rais Jacob Zuma kujiuzulu mara moja.  Katika mkutano mapema leo, baraza la kitaifa la chama hicho kimeamua kwa kauli moja kumpa nafasi Zuma ajiuzulu.  Japo kuna hisia kuwa huenda zuma akakaidi agizo hilo ambalo kwa sasa limesalia na saa ishirini na nne kutekelezwa, ANC imesema itachukua hatua zaidi kuhakikisha ameng'atuka.  Zuma alipoteza nafasi yake kama kiongozi wa chama hicho huku naibu wake wa Rais Cyril Ramaphosa akimrithi.