Jaji Kihara Kariuki ateuliwa mwanasheria mkuu nchini baada ya Profesa Githu Muigai kujiuzulu

KTN Leo | Tuesday 13 Feb 2018 7:12 pm

Jaji Kihara Kariuki ndie sasa ameteuliwa mwanasheria mkuu nchini Kenya baada ya profesa Githu Muigai kujiuzulu wadhifa wake. Profesa Muigai anaondoka ofisini baada ya kuhudumu kama mwanasheria mkuu nchini kwa muda wa miaka sita unusu. Rais Uhuru Kenyatta akitangaza kupokea barua ya kujiuzulu kwake Muigai aidha ametangaza uteuzi wa maafisa wengine kadhaa watakaohudumu kwa muhula wake wa pili wa uongozi.