Jukwaa la KTN: Msasa wa mawaziri

KTN Mbiu | Monday 12 Feb 2018 6:37 pm

Mawaziri wote tisa wateule waliofanyiwa mchujo juma lililopita wameidhinishwa na kamati ya bunge kuhusu uteuzi. Hata hivyo, ripoti ya kamati hiyo inatarajiwa kujadiliwa bungeni wakati ambapo bunge litakapokuwa likirejelea vikao. Haya yanajiri huku Rais Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto wakiandaa kikao ikulu kesho asubuhi kwa lengo la kujiandaa kwa waakilishi wake bunge linaporejelea vikao.