Wakili wa Miguna Miguna watoa malalamiko kotini kuhusu kufurushwa kwake Miguna

KTN Mbiu | Wednesday 7 Feb 2018 4:54 pm

Mkuu wa polisi, Joseph Boinett na kaimu mkurugenzi wa idara ya upelelezi, George Kinoti, wameamuriwa kuwasilisha hati ya kiapo mahakamani kufikia ijumaa hii ili kubaini na kueleza ni vipi Miguna Miguna alisafirishwa kutoka nchini, ilihali mahakama kuu ilikuwa imeagiza aachiliwe huru. Jaji wa mahakama kuu, Luka Kimaru, ametoa agizo hilo kufuatia ombi la mawakili wake Miguna Miguna, walioikashifu serikali kwa kuipuuza mahakama.