.
28th January, 2018
Utata umeendelea kuigubika bustani ya Uhuru, Nairobi
ambako muungano wa NASA umesisitiza kuwa utaandaa hafla
ya kumuapisha Raila Odinga na Kalonzo Musyoka siku ya
jumanne. Hata hivyo, serikali hii leo kupitia kamanda wa
polisi japehth koome imesisitiza kuwa hakuna mkutano
wowote utakaoandaliwa katika eneo hilo. Na kama
mwanahabari wetu wa masuala ya siasa Jeff Kirui
anavyotuarifu, NASA inashikilia kuwa imejiandaa kwa hafla
hiyo licha ya naibu rais William Ruto kuongoza Jubilee
kusisitiza kuwa hawautambui uapisho huo.