Swala la kuapisha kinara wa NASA Raila Odinga kama rais zashika kasi: Mirindimo

Dira ya Wiki | Friday 26 Jan 2018 7:52 pm

Spika katika bunge la kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi amewataka viongozi wa upinzani kufanya hima ili kurejesha amani na uwiano nchini. Elachi vile vile ameeleza hisia zake kufuatia uapisho wa Raila Odinga juma lijalo na kusema kuwa hautakuwepo huku akishikilia kuwa amani ni muhimu nchini. Alizungumza baada ya kufanya mkutano na baadhi ya viongozi vijana kutoka kati mwa Kenya.