Rais Uhuru Kenyatta awateua baraza lake la mawaziri

Dira ya Wiki | Friday 26 Jan 2018 7:25 pm

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza baraza lake lote la mawaziri huku baadhi ya waliohudhumu katika muhula wake wa kwanza wakiondolewa katika baraza lake jipya ambalo linatakiwa kupata idhini ya bunge kabla kuanza kuhudumu. Nyadhifa nyingine mpya zilibuniwa kama vile katibu msimamizi katika wizara. Miongoni mwa majina mapya katika baraza hilo la mawaziri yanajumuisha waziri wa jinsia profesa Margaret Kobia, waziri wa ardhi bi. Farida Karoney ambaye ni msimamizi mkuu wa shirika la habari la Royal Media na Rashid Mohamed ambaye ni waziri wa michezo. Baadhi ya mawaziri wamehamishwa na kuwa mabalozi katika nchi mbalimbali kama vile Dan Kazungu, Cleopa Mailu na profesa Jacob Kaimenyi.