Wanasiasa wa muungano wa NASA waendelea kuhamasisha wananchi kwa uapishaji wa Raila na Kalonzo

Dira ya Wiki | Friday 19 Jan 2018 7:53 pm

Viongozi wa NASA Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wanaendelea kushinikizwa kuapishwa kuwa rais wa watu wa Kenya na naibu wake. Katika mkutano uliofanywa huko Machakos wa kuhamasisha watu kuhusu bunge la mwananchi wanasiasa wa NASA waliwataka viongozi hao kutoyumbayumba kuhusu suala la kuapishwa. Katika hafla hiyo Raila Odinga alisistiza kuwa mpango wa kuwaapisha mwishoni mwa mwezi huu ungalipo