Watu watano wafariki katika maeneo ya Sigalagala kwa barabara ya Kakamega-Kisumu

Dira ya Wiki | Friday 12 Jan 2018 7:51 pm

Watu watano wamefariki katika ajali ya barabarani katika eneo la sigalagala kwenye barabara ya Kakamega ? Kisumu ajali hiyo iliyotukia jana usiku ilihusisha gari dogo na pikipiki. Waliofariki walikuwa wamebebwa kwenye pikipiki moja wakati wa ajali hiyo ambapo gari hilo na pikipiki ziligongana ana  kwa ana. Abiria wa bodaboda hiyo walikuwa wakielekea kwa mazishi ya jamaa wao katika eneo la musingu. Hali ya huzuni ilitanda katika kijiji hicho huku wenyeji wakiomboleza kufariki kwa watu hao wa familia moja .