.
4th December, 2016
Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli amemuomba Rais Uhuru Kenyatta kuchukuwa msimamo mkali dhidi ya wafisadi nchini. Akiandamana na mbunge wa Lugari Ayub Savula, Atwoli amesema kuwa visa vya ufisadi vimekithiri nchini ilhali Rais anaonekana kulegeza kamba. Atwoli aliyasema haya katika kanisa Katoliki la Manyonyi Lugari katika hafla ya kuchangisha hela.